.

.

.

Monday, September 16, 2013

Vinyago vya tangaza Utamaduni wa Kiafrika


 Katika muda mrefu uliopita uhusiano kati ya China na nchi za Afrika ulikuwa ukihusisha serikali za pande mbili. Lakini mwelekeo huo kwa sasa unaendelea kubadilika, mbali na serikali kushughulikia mambo ya ushirikiano, watu binafsi pia wanashiriki katika kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili.
Bw. Li Songshan ni raia wa China na ameishi nchini Tanzania kwa miaka mingi. Yeye hutumia vinyago kuonyesha utajiri wa utamaduni wa kiafrika nchini China ili kukuza uhusiano kati ya pande hizo mbili. Bw Li Songshan na mkewe wameandaa maonyesho ya vinyago kutoka nchini Tanzania na nchi nyingine za kiafrika yaliyoanza Machi 12 hadi Aprili 12 ili kuwaonyesha wachina utamaduni wa kiafrika.
Tulipofika kwenye maonyesho hayo hapa mjini Bejing wilayani Tongzhou, tulikaribishwa vizuri na Bw Li Songshan na mkewe. Ndani ya jumba hilo kulikuwa na
watu wengi waliofika kujionea vinyago hivyo vilivyochongwa kuonyesha maisha ya kawaida ya waafrika. Lakini ni kitu gani kilichomchochea Bw Lishuan na mkewe kufanya hivyo?

Bw. Li Songshan
Mbali na Tanzania, vinyago vingine vilinunuliwa nchini Zambia, Malawi na Msumbiji.Akifungua maonyesho hayo, balozi wa Tanzania nchini China Bw Mapuri anasifu juhudi za Bw Li Songshan na mkewe za kuendeleza urafiki wa pande hizo mbili.Anasema maonyesho hayo yana umuhimu mkubwa sana kwa Tanzania na Afrika kwa jumla.

Balozi Mapuri
Safari ya kutafuta vinyago ya Bw Lishuan na mkewe ilianzia Mtwara nchini Tanzania ambako walijumuika na jamii ya wamakonde wanaosifiwa kwa uchongaji vinyago nchini humo.Bi. Han anasema ukarimu wa jamii ya wamakonde uliwafanya washirikiane katika kubuni chama cha uchongaji vinyago cha jamii hiyo, yaani "Makonde welfare Association" ambacho kimesaidia kuwatafutia masoko ya vinyago vyao.

Bi Han Rong
Kwenye maonyesho hayo kulikuwa na watu wengi wakiwemo wanafunzi hawa wa kichina waliotaka kujifunza maneno machache ya lugha ya Kiswahili. Wanasema, waliamua kuhudhuria maonyeshon hayo kwa kuwa wanapenda sana utamaduni wa kiafrika na wamefika kujua mengi zaidi kuhusu Afrika.

Wanafunzi
Mbali na vinyago, pia kuna Leso na picha zinazoonyesha mwanzo wa juhudi za Bw Lishuan na mkewe katika kukuza uhusiano wa pande hizo mbili. Leso zilizogusa macho ya wengi ni zile zilizokuwa na picha za mwanzilishi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na rais wa sasa wa jamhuri ya watu wa China Hu Jintao. Tukiwa ndani tulijawa na shauku ya kutaka kujua iwapo vinyago hivyo vitauzwa baadaye au la. Lakini Bi Han anasema hawataviuza. Badala yake watajenga jumba la maonyesho na kuvihifadhi ili wachina waendelee kujua mengi kuhusu Afrika.

Bi Han Rong 
Tulipokuwa tukiondoka, Bw Lishuan alikuwa na ushauri mmoja kwa waafrika hususan wakazi wa Afrika mashariki na kati.

Bw Li Songshan
Mwaka wa 2003, Bw na Bi Li Songshan walifaulu kujenga jumba la maonyesho ya sanaa katika mkoa wa changchun, kaskazini mashariki mwa China ambalo hadi kufikia sasa limewavutia zaidi ya watu milioni 5.Safari hiyo ya Bw na Bi Li Songshan ya kutafuta na kujenga urafiki kati ya waafrika na wachina imewafanya kuiga baadhi ya mambo ya kiafrika na kuyafanya kuwa desturi maishani mwao. Wawili hao, wanajivunia sana baadhi ya mambo hayo ikiwemo lugha ya Kiswahili ambayo ni sehemu ya utamaduni wa kiafrika.

No comments:

Post a Comment